

MWANDISHI: Wewe unawalisha ng'ombe chakula gani?
MKULIMA: Ng'ombe yupi Mweupe au Mwekundu?
MWANDISHI: Ng'ombe mweupe
MKULIMA: Ninamlisha nyasi na viguta vya mahindi
MWANDISHI: Na mwekundu?
MKULIMA: vilevile nyasi na viguta vya mahindi
MWANDISHI: ahaa sawa,na sehemu ya kulala ni wapi?
MKULIMA: Ng'ombe yupi mweupe au mwekundu?
MWANDISHI: Mweupeee!!!!
MKULIMA: Mweupe ninamlaza bomani kulee
MWANDISHI: na mwekundu?
MKULIMA: vile vile namlaza na mwenziwe.
MWANDISHI: Hii sehemu yote majumba mengi wakati wa kulisha unafanyaje?
MKULIMA: Yupi mweupe au mwekundu?
MWANDISHI: Woooteeee!!!! {kwa hasira}
MKULIMA: Mweupe ninamfunga kamba na kumzungusha malishoni na kumrudisha
MWANDISHI: Na mwekundu vilevile?
MKULIMA: Mwekundu? Mwekundu yeye ninamfunga kamba na kuzunguka naye kama mwenziwe tu.
MWANDISHI: Kwanini kila mara nikikuuliza kuhusu huduma za ng'ombe wako unaniuliza mweupe au mwekundu halafu inatokea kuwa wote unawapa huduma sawa?????
MKULIMA: Kwa sababu ng'ombe mweupe ni wangu,
MWANDISHI: Na mwekundu?
MKULIMA: Na mwekundu vile vile ni wangu.